Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Mexico: Mkuu wa jiji la Iguala asakwa na vyombo vya sheria

Maelfu ya raia wa Mexico wameandamana Jumatano Oktoba 22 katika barabara za miji muhimu ya nchi hiyo wakiomba mwanga utolewe kuhusu wanafunzi 43 wa chuo kikuu cha Ayotzinapa ambao hawajulikani walipo tangu walipokamatwa na polisi.

Watu waliojificha nyuso walichoma jengo la manispaa ya Iguala, Jumatano, Oktoba 22.
Watu waliojificha nyuso walichoma jengo la manispaa ya Iguala, Jumatano, Oktoba 22. REUTERS/Jorge Dan Lopez
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Mexico, wanafunzi na wazazi wa wanafunzi waliyotekwa waliandamana katika eneo la kihistoria wakiomba mkuu wa jimbo la Guerrero ajiuzulu.

Waandamanaji wamekua wakiomba serikali kufanya kiliyo chini ya uwezo wake ili wanafunzi 43 ambao hawajulikani walipo wapatikane wakiwa hai, huku wakiomba sheria ifuate mkondo wake.

Waandamanaji hao wameomba pia vyommo vya sheria kuwahukumu Askari polisi wa Iguala, ambao walishirikiana na kundi la wahuni wanaotumia madawa ya kulevya kwa kuwaua wanafunzi watatu na kuwateka wanafunzi wengine 43 wa chuo kikuu cha Ayotzinapa

Wakati huohuo, jengo la serikali, ambalo ni makao makuu ya manispaa ya jiji la Iguala limechomwa moto, wakati ambapo mkuu wa jiji hilo haijulikani aliko. Hata hivo hiyo Mkuu huyo wa jiji la Iguala anatafutwa na vyombo vya sheria, baada ya hati ya kukamatwa kutolewa.

Mwendesha mashtaka wa taifa alithibitisha Jumatano Oktoba 22 kwamba Mkuu huyo wa jiji na mkewe ndio waliamrisha kutekwa kwa wanafunzi hao. Watu hao walikua na uhusiano wa karibu na kundi la wahuni wanatumia madawa ya kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.