Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: wahusika katika mauaji ya watu zaidi ya 80 waanza kukamatwa

Waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Richard Muyej Mangez, ametangaza kuwa baadhi ya wahusika wa mauaji ya watu zaidi ya 80 katika miji ya Beni na Eringeti wameanza kukamatwa.

Waziri wa mambo ya ndani, Richard Muyej, akiwasili Beni Oktoba 19 mwaka 2014.
Waziri wa mambo ya ndani, Richard Muyej, akiwasili Beni Oktoba 19 mwaka 2014. AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri huyo, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijatupilia mbali pendekezo la kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa lililotolewa na baadhi ya wanasiasa, na kusema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wahusika wote katika mauaji hayo watakuwa wamekamatwa.

Tamko hilo la waziri wa mambo ya ndani linakuja siku moja baada ya kiongozi wa chama cha upinzani cha RCD-KML chenye umaarufu mkubwa katika mji huo wa Beni,Mbusa Nyamwisi, kuelezea kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na waasi wa Uganda wa kundi la ADF-NALU ambao walishirikiana na baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo ya Congo.

Mamia ya raia wa Beni wakiandamana mbele ya ofisi ya tume ya Umoja wa Mataifa Monusco, Jumatano Oktoba 22.
Mamia ya raia wa Beni wakiandamana mbele ya ofisi ya tume ya Umoja wa Mataifa Monusco, Jumatano Oktoba 22. REUTERS/Kenny Katombe

Matamshi hayo kama alivosema waziri Muyej, yanalenga kuzusha uhasama kati ya raia wa eneo la mashariki mwa Congo na viongozi wao, upande mmoja lakini kutaka kuwafanya wananchi wasiwe na imani na Jeshi lao, licha ya kuwa operesheni za kuwatimua wapiganaji hao wa ADF-Nalu zikiendelea.

Hayo yanajiri wakati rais Joseph Kabila Kabange anazuru eneo hilo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia mjini Kisangani, mkoa wa Mashariki ambako amezindua mradi wa ujenzi wa daraja kuu linalounganisha mkoa wa Mashariki na Katanga, na hivi sasa wananchi wa Beni wanatarajia kumpokea rais huyo, ambaye kwa mujibu wa itifaki anakuja kuwapa pole wananchi wa eneo hilo kufwatia mauaji ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.