Pata taarifa kuu
LIBANON-Usalama

Libanon: jeshi laurejesha mji wa Tripoli kwenye himaya yake

Wanajeshi wa Lebanon wameudhibiti mji wa Tripoli uliokuwa umekaliwa na wapiganaji wanaoshirikiana na kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Mwanajeshi wa Libanon akiwa katika ya Bab el-Tebbané mjini Tripoli, Oktoba 27 mwaka 2014.
Mwanajeshi wa Libanon akiwa katika ya Bab el-Tebbané mjini Tripoli, Oktoba 27 mwaka 2014. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji hao yamesababisha watu 16 na maelfu kukimbia makwao tangu siku ya Ijumaa juma lililopita.

Jeshi limesema limewakamata wapiganaji 162 na kuwataka wengine kuacha mapigano na kuweka silaha zao chini.

Wapiganaji hao wanasema wanataka jeshi kusitisha operesheni dhidi yao.

Jeshi Libanon lilianza kuingia katika kata ya Bab el-Tebbané Jumatatu Oktoba 27, baada ya raia kuondoka katika kata hiyo, ambayo ilikua makao makuu ya waasi wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.