Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Mazungumzo ya Nyuklia ya Iran huenda yakatamatika hii leo

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif anarejea hii leo jijini Vienna Uswisi baada ya siku moja ya mashauriano jijini Teheran ambapo huenda makubaliano yakafikiwa hii leo kuhusu mzozo wa nyuklia wa Iran.

waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammed Javaz Zarif
waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammed Javaz Zarif
Matangazo ya kibiashara

Jambo moja ambalo linaonekana katika sakata hili lililoanza miezi 20 iliopita tarehe ya mwisho kufikia makubaliano ya kihistoria hii Jumanne Juni 30, itavuka bila kufikia makubaliano. Hakuna kikomo kingine kilichowekwa ingawaje uwezekano wa kuongeza muda zaidi umewekwa kando.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema bado ni mapema kuzungumzia matokeo ya majadiliano, wakati ambapo swali nyeti bado halijatatuliwa.

Javaz Zarif anakutana mjini Vienna na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi zenye nguvu duniani akiwemo John Kerry wa Marekani, baada ya kufanya mashauriano ya kidiplomasia na viongozi wa serikali ya Iran ambapo katika mazungumzo ya awali hapakuwa na tathimini yoyote kuhusu mazungumzo hayo iwapo yalikuwa hasi au chanya.

Tayari mawaziri wa serikali za nchi nchi 5+1 zenye nguvu wapo Vienna kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo hayo ambayo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond amesema wanaelekea kuchukuwa maamuzi magumu.

Iran na nchi 5+1 zimeanza mazungumzo tangu miezi 20 sasa kutafuta muafaka juu ya swala la Nyuklia ya Iran ambapo Iran inatuhumiwa kutumia Nyuklia kwa ajili ya kutengeneza silaha za maangamizi, jambo ambalo linatupiliwa mbali na serikali ya Teheran ambayo inasema matumizi yake ni ya manufaa kwa maendelea ya wananchi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.