Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Zimbabwe yatangaza hali ya dharura nchi nzima kutokana na ukame

Rais wa Zimbabwe ametangaza hali ya dharura kitaifa kwenye baadhi ya maeneo ya nchi ambayo yamekumbwa na ukame na wananchi wanahitaji haraka chakula cha msaada.

Mkulima akilima eneo ambalo limekumbwa na ukame na mazao kudumaa, Zimbabwe imetangaza hali ya dharuraize crop.
Mkulima akilima eneo ambalo limekumbwa na ukame na mazao kudumaa, Zimbabwe imetangaza hali ya dharuraize crop. Photo: Howard Burditt/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake rais Mugabe amesema kuwa hali ya ukame iliyokumba maeneo mengi ya nchi inatishia ustawi wa jamii, na ndio maana ameamua kutangaza hali ya dharura kunusuru raia.

Rais Mugabe ameongeza kuwa maeneo mengi ya nchi hasa yale ya vijijini wananchi wake wanakabiliwa na njaa, na kwamba chakula cha msaada kinahitajika kupelekwa kwenye maeneo hayo.

Akisoma tangazo la rais, waziri wa Serikali za mitaa na kazi, Saviour Kasukuwere, amesema kuwa watu milioni zaidi ya milioni mbili hawana chakula ambayo ni sawa na asilimia 26 ya raia wake.

Tangazo hili linatolewa ikiwa ni majuma kadhaa yamepita toka shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP litoe ripoti kuhusu mwenendo wa chakula duniani na kuitaja nchi ya Zimbabwe kuwa miongoni mwa mataifa yaliyoathirika na ukame.

Mazao yakiwa yamenyauka nchini Zimbabwe kutokana na ukame
Mazao yakiwa yamenyauka nchini Zimbabwe kutokana na ukame ALEXANDER JOE / AFP

Ripoti ya WFP iliongeza kuwa sababu kubwa ya maeneo mengi ya nchi kukumbwa na ukame ni pamoja na mvua za Elnino zilizonyesha na kuendelea kunyesha kwenye maeneo mengi ya nchi za kusini mwa Afrika ambazo zimeharibu mazao.

Kabla ya tangazo hili Serikali ilikanusha maeneo mengi kuwa na uhaba wa chakula, lakini sasa inaonekana kubadili kauli yake na kutangaza hali ya dharura nchi nzima.

Rais Mugabe amelaumu hali hiyo kuchangiwa na wakulima kutofanya kilimo cha kisasa lakini pia mabadiliko ya tabia nchi pamoja na vikwazo ilivyowekewa nchi yake na nchi za magharibi.

Wakosoaji wa Serikali wanadai kuwa tatizo hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na sera ya Serikali kuhusu ardhi ambayo ilipitishwa na bunge mwaka 2000 wakati serikali ilipoamua kuwafukuza wakulima wakizungu.

Waziri Kasukuwere amesema kuwa karibu ngombe na ndama elfu 16 wamekufa nchi nzima kutokana na ukame huku asilimia 75 ya mazao yakiachwa bila kuvunwa pamoja na ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.