Pata taarifa kuu
SYRIA-MIKUTANO - MUNICH

Mashambulizi zaidi yashuhidiwa nchini Syria huku mkutano wa amani ukizinduliwa mjini Munich

Mkutano wa kimataifa unazinduliwa hii leo kuhusu Syria, huku kukiwa hakuna matumaini yoyote ya kupatikana kwa muafaka baada ya kufeli kwa hatuwa za awali za mazungumzo. Hayo yanajiri wakati huu jeshi la serikali ya Damascus linalosaidiwa na majeshi ya Urusi likiendelea na mashambulizi mashariki mwa Syria.

Mashambulizi katika mji wa Aleppo nchini Syria
Mashambulizi katika mji wa Aleppo nchini Syria REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Damascus inayosaidiwa na ndege za kivita za Urusi imeendeleza mashambulizi katika mji wa Aleppo na kusababisha watu kuendelea kukimbia zaidi makaazi yao wakihofia usalama wao.

Hayo yanajiri wakati huu serikali ya Urusi ikitangaza kuwa tayari kufanya majadiliano kihusu usitishwaji wa mashambulizi ya anga nchini Syria kulingana na masharti ya waasi na nchi za magharibi zinazolaumu mashambuliz hayo kuwa sababu za kufeli kwa mazungumzo ya amani ya huko Geneva Uswisi.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Guennadi Gatilov, amesema wapo tayari kujadiliana kuhusu mikakati ya kusitisha mashambulizi nchini Syria, na wanaelekea katika mkutano wa kimataifa kuhusu Syria mjini Munich na swala hili litajadiliwa.

Marekani na washirika wake wanajaribu kuishinikiza Urusi hii leo katika mkutano wa mawziri wa mambo ya nje pamoja na wadau muhimu katika mgogoro wa Syria huko Munich kuhusu mashambulizi yake nchini Syria.

Mkutano huo wa kimataifa unaenda kuwa kichocheo cha kuzindua upya mazunguzo ya amani kati ya utawala wa Damascus na upinzani baada ya serikali ya rais Assad kuzidisha mashmbulizi ya anga katika ngome za waasi chini ya usaidizi wa Urusi.

Kwa sasa inasubiriwa kuona iwapo mazungumzo yatazinduliwa tena upya Februari 25 mwaka huu. Serikali ya Damascus ipo tayari kwa mazungumzo wakati wowote huku upinzani ukiendelea kutia ngumu kwa kutowa masharti kadhaa ikiwemo kusitishwa kwa mashambulizi ya ndege za Urusi zinazo yasaidia majeshi ya Assad kusonga mbele kwenye uwanja wa mapambano.

Nchi za magharibi zinaitaka Urusi kusitisha mashambulizi yake ya anga yaliosababisha maelfu ya watu kuyatoroka makaazi yao tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari katika jimbo la Aleppo.

Urusi imekuwa ikitetea mashambulizi hayo kuwa halali kwani yamekuwa yakilenga mgome za magaidi na imeahidi kutowa mapendekezo mapya ili kupiga hatuwa nyingine kuhusu swala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.