Mbunge maalum nchini Kenya Sheikh Mohammad Dor atiwa nguvuni

Mbunge maalum nchini Kenya Sheikh Mohammad Dor alitiwa nguvuni mapema hii leo kutokana na matamshi aliyoyatoa juma lililopita kuhusu ufadhili wa kundi la Mombasa Republican council, linalopigania kujitenga na taifa la Kenya. Mbunge huyo amekamatwa asubuhi ya leo kutoka nyumbani kwake.
Mbunge huyo alitamka kwamba kundi la MRC liendelee kutafuta pesa na waendelee na shughuli zao, iwapo watafika kwake, kuomba ufadhili, atakuwa tayari kuchangia. Matamshi hayo alioyatowa wakati akizundua shughuli za chama chake cha kisiasa jijini Mombasa Juma lililopita, ndio ambayo yamepelekea kukamatwa kwake na kuwekwa korokoroni.
kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja siku chache baada ya kiongozi wa idara ya upelelezi kudokeza kuwa wanasiasa watatu pamoja na wafanyabiashara wawili wanachunguzwa kutoka na madai ya kufadhili kundi la MRC kuzua vurugu.
Mwezi Agosti mahakama kuu mjini Mobmasa ilifutilia mbali uharamu wa kundi la MRC, jambo ambalo serikali ya Kenya haikulifurahia na kusisitiza kuwa itakata rufaa.
Cheikh Mohamed Dor aliona kuwa kundi la MRC halijakiuka katiba na linastahili kuungwa mkono na kila mmoja, kwakuwa mahakama haijakiharamisha chama hicho.
Kundi la MRC limehusishwa na maswala ya ukiukwaji wa sheria katika eneo la Pwani, huku likikashifiwa kuwa linapanga kuvuruga mitihani ya kitaifa, pamoja na uchaguzi mkuu ujao.
Licha ya watu wawili kufariki siku ya Jumatatu asubuhi wakati jeshi la polisi lililopo vamia makaazi ya kiongozi wa kundi hilo jijini Mombasa, huku serikali ikisisitiza kuwa itakabiliana na kundi hilo hadi hali ya kawaida irejee.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya