Pata taarifa kuu
Zanzibar - Uchaguzi

Rais wa Tanzania aunga mkono kurejewa kwa uchaguzi Zanzibar

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameunga mkono kurejewa kwa uchaguzi mkuu wa rais visiwani Zanzibar, licha ya upinzani kutangaza kususia uchaguiz huo huku jamii ya Kimataifa ikitiwa wasiwasi na hali huenda ikazua machafuko mapya kisiwani humo.

waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda, Augustino Mahiga akizungumza mbele ya wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania Februari 8, 2016
waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda, Augustino Mahiga akizungumza mbele ya wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania Februari 8, 2016
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi uliofanyika mwaka uliopita katika kisiwa hicho cha Tanzania, ulifutwa na tume ya uchaguzi, ilioleza kwamba uchaguzi huo umegubikwa na wizi wa kura, jambo ambalo liliwatia hofu wanadiplomasia wa nchi 15 za kigeni nchini Tanzania.

Hatuwa hiyo ilikuja baada ya kiongozi wa upinzani wa chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad kudai kuwa ndie alieshinda uchaguzi huo dhidi ya mgombea wa chama cha CCM Dk Ali Mohamed Shein

Hata hivyo rais Magufuli anaona kwamba njia muafaka ya kutatua mzozo wa kisiasa viziwani Zanzibar ni kurejelewa kwa uchaguzi.

Rais Magufuli amesema katika hotuba iliosomwa jana na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na kikanda, Augustino Mahiga mbele ya mabalozi wanaowakilisha nchini zao nchini Tanzania, njia muafaka ya kutatua mzozo wa Zanzibar ni kurejelea uchaguzi.

Octoba 25 ulifanyika uchaguzi nchini Tanzania, sambamba na visiwani Zanzibar, lakini baadae tume ya uchaguzi ya Zanzibar ilitangaza kufuta uchaguzi huo baada ya kiongozi wa upinzani kutoka chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad kujitangaza kuwa mshindi kabla hata ya matokeo rasmi kutangazwa.

Chama cha CUF kilitangaza kuwa kitasusia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika March 20 mwaka huu.

Magufuli amesema kususia uchaguzi kwa chama hicho hakutowi ishara njema kwa amani na utulivu visiwani Zanzibar, na kuongeza kwamba juhudi za usuluhishi kutafuta muafaka zilizoanza tangu mwezi Novemba mwaka haba ziligonga mwamba.

Matukio kadhaa ya vurugu na milipuko ya guruneti ilishuhudiwa visiwani humo miaka iliopita, na kutikisa sekta ya Utalii ambayo ni muhimu visiwani humo.

Mabalozi wa nchi 15 wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakiwemo Umoja wa Ulaya na Marekani wamesema matumaini makubwa yalikuwa ni kupatikana kwa muafaka wa mzozo huo wa kisiasa visiwani Zanzibar kwa njia ya mazungumzo

Hivi karibuni tume ya uchaguzi visiwani humo ilitangaza kurejelewa kwa uchaguzi March 20, hatuwa ambayo wanadiplomasia wanasema inatia wasiwasi wa kutokea kwa vurugu.

Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wa chama cha Mapinduzi CCM cha rais Magufuli atasalia kuwa madarakani hadi pale uchaguzi utapofanyika.

Rais magufuli amewatolea wito upinzani kushiriki kwenye uchanguzi huo na kutoususia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.