Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Riek Machar apewa tarehe ya mwisho

Mataifa ya Magharibi, yanamtaka kiongozi wa waasi Riek Machar nchini Sudan Kusini kufika jijini Juba hadi Jumamosi hii Aprili 23 ili kuunda serikali ya pamoja na rais Salva Kiir.

Kiongozi wa waasi Riek Macharaendelea kusubiriwa Juba.
Kiongozi wa waasi Riek Macharaendelea kusubiriwa Juba. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mvutano wa silaha na wanajeshi zaidi wa kiongozi huyo wa waasi, na serikali ya Juba umeendelea kuchelewesha kuwasili kwa kiongozi huyo anayesubiriwa pia na raia wa nchi hiyo.

Waangalizi wa utekelezwaji wa mkataba wa amani nchini Sudan Kusini wanaonya kuwa kutorejea kwa kiongozi wa waasi Riek Machar jijini Juba, kuna hatarisha ya kuzuka tena kwa mapigano nchini humo.

Mwenyekiti wa Waangalizi hao ambaye ni rais wa zamani wa Boswtana Festus Mogae anasema, ikiwa Machar hatafika Juba hivi karibuni kuna uwezekano mkubwa wa kuanza tena kwa mapigano nchini humo na kuvunjika kabisa kwa mkataba wa uundwaji wa serikali ya pamoja, serikali ambayo Riek Machar atakuwa Makamu wa kwanza wa rais.

Wasiwasi huu pia umeonyeshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi juma hili, kwa hatua ya kutowasili kwa Machar huku Marekani ikimshutumu kiongozi huyo wa waasi kwa kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza mkataba huo uliofikiwa mwaka jana.

Lakini swali kubwa ni kwanini Machar hajarejea? Serikali ya Juba na waasi wanalaumiana kwa kutowasili Machar.

Waasi wanasema, serikali ya Juba imekataa kiongozi wao awasili. Serikali ya rais Kiir inasema wanajeshi wa waasi ambao tayari wako Juba ni 1,370 idadi ambayo serikali inasema inatosha na hivyo hakuna haja ya kuwasili kwa mamia ya wapiganaji wengine wa waasi, madai ambayo Riek Machar anatupilia mbali.

Machar anasema mkataba wa amani unamruhusu kuja na wanajeshi 2,910 na yeye anataka tu kuandamana na wanajeshi 260 na anasisitiza kuwa yuko tayari kufika Juba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.