Iran-Nyuklia - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 25 mei 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 25 mei 2012

Baada ya mkutano wa Bagdad Iran na mataifa tajiri kukutana jijini Moscow

Saeed Jalili, anafuatilia majadilino baina ya Iran na mataifa tajiri
Saeed Jalili, anafuatilia majadilino baina ya Iran na mataifa tajiri
REUTERS/Thaier al-Sudani

Na Ali Bilali

Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani yamefanikiwa kwa kiasi kidogo katika mkutano wao wa siku mbili juu ya maswala ya Nuklia Mazungumzo yaliyofanyika mjini Baghdad nchini Iraq.

Mataifa hayo yamekubaliana kukutana tena jijini Moscow nchini Urusi tarehe 18 na 19 mwezi ujao ili kuendelea na mazungumzo yao.

Mkuu wa Sera za kigeni ndani ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kuwa wanaendelea kuwa na imani kuwa wataweza kufikia muafaka siku za karibuni kupitia mazungumzo, na kuahidi kuwa watafanya juhudi mpaka mwisho.

Hatahivyo ametanabaisha kuwepo kwa hali ya kutokubaliana na kuitaka Iran kutekeleza hatua zilizopendekezwa na Jumuia ya kimataifa.
Ashton aliweka mapendekezo mapya mezani kwa niaba ya mataifa hayo, Mapendekezo ambayo hayakuridhiwa na Iran

Mataifa hayo yametaka Irana kupunguza mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium kwa asilimia 20, mpango ambao mataifa hayo yamehofu kuwa Iran inampango wa kutengeneza silaha za hatari.
 

tags: Iran - Marekani - Ufaransa
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close