Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA

Mazungumzo kati ya M23 na ujumbe wa Serikali ya DRC yan'goa nanga mjini Kampala, Uganda

Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC kwenye mazungumzo ya Kampala kati yake na waasi wa kundi la M23 tayari wamewasili nchini Uganda ambapo sasa wanasubiri kupatiwa ajenda za mazungumzo yao.

Mratibu wa mazungumzo ya Kampala na waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga
Mratibu wa mazungumzo ya Kampala na waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa DRC, Francois Mwamba anasema kuwa wenyewe wako tayari kwa mazungumzo hayo yatakayodumu kwa siku kumi na nne na kwamba wanasubiri kutolewa kwa ajenda na mratibu wa mazungumzo hayo ambayo ni Serikali ya Kampala.

Akifanya mahojiano maalumu na kituo chetu cha RFIKISWAHILI Francois Mwamba anasema kuwa hakuna madai mapya yaliyowasilishwa na waasi wa M23 na kwamba yote walioyasema juma hili yalikuwemo kwenye mazungumzo yaliyovunija hapo awali.

Hata hivyo kiongozi huyo ameongeza kuwa wao kama Serikali wako tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa na nchi za ukanda wa maziwa makuu kuwafurusha wapiganaji wa kundi la FDLR ambao waasi wa M23 wanataka waondoke nchini humo pamoja na kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa kongo walioko nchini Uganda na Burundi.

Hata hivyo mratibu wa mazungumzo haya ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga amethibitisha kuanza kwa mazungumzo haya na kuongeza kuwa wanamatumaini makubwa kuwa watapiga hatua na kufikia maridhiano.

Pande hizo mbili zina siku 14 kuhakikisha wanafikia muafaka kwenye mazungumzo hayo kabla ya viongozi wa nchi kumi na moja za maziwa makuu hawajapewa ripoti ya mazungumzo hayo na kuangalia hatua za kuchukua kumaliza mzozo wa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.