Syria - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatano 05 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 05 septemba 2012

Takriban watu 19 wauawa baada ya Vikosi vya Syria kushambulia mji wa Aleppo unaodhibitiwa na Waasi

Rais wa Syria,Bashar Al Assad
Rais wa Syria,Bashar Al Assad
DR

Na Lizzy Anneth Masinga

Watu 19 wameuawa wakiwemo watoto saba baada ya Vikosi vya nchini Syria kufanya Mashambulizi katika Mji unaodhibitiwa na Waasi, Aleppo Alfajiri ya leo, Shirika linalotetea haki za Binaadam nchini Syria limeeleza.

Wanaharakati wameripoti kuwa Mashambulizi ya Mara kwa mara na upungufu wa Chakula katika maeneo ya karibu na Damascus, huku hali ikiripotiwa kuwa shwari katikati ya mji huo.
 

Mpatanishi Mpya wa Mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi ameonya kuwa hali ya mambo ilivyo nchini Syria inaendelea kuwa mbaya zaidi.
 

Kauli yake imekuja wakati Mkuu wa Kamati ya Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu Peter Maurer alipoanza Operesheni nchini Syria, Operesheni yenye lengo la kulinda Raia huku Shirika la kimataifa linaloshughulikia Wakimbizi UNHCR kudai kuwa Takriban watu laki moja wameikimbia nchi hiyo mwezi August pekee.
 

Waangalizi wa haki za Binaadam nchini Syria wanajiegemeza katika Ripoti ya Mtandao wa Wanaharakati , wakisema kuwa zaidi ya Watu 26, 000 wameuawa nchini Syria tangu kuanza kwa Maandamano ya kumtaka Rais wa Nchi hiyo Bashar Al Assad kuondoka Madarakani Mwezi March Mwaka jana.
 

tags: Syria
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close