SYRIA -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 22 septemba 2012 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 22 septemba 2012
Majeshi ya Syria yakabiliana na waasi jirani na kambi ya Aleppo
moja kati ya makabiliano yanayoendelea nchini Syria baina ya majeshi huru ya Syria dhidi ya majeshi ya serikali
Reuters/Goran Tomasevic
Waangalizi wa amani nchini Syria wameeleza kuzuka kwa mapigano baina ya majeshi ya Syria yakisaidiwa na ndege za kivita dhidi ya waasi mjini Aleppo jirani na uwanja wa ndege wa kijeshi.
Mjini Damascus shirika la habari limearifu jeshi la Syria limebaini maiti 25 za watu waliouawa wilaya ya Qadam na kulaumiwa makundi ya kigaidi yanayomiliki silaha kwa kutekeleza mauaji hayo.
Katika muendelezo wa mauaji mtu mmoja aliyeficha uso wake kwa kivazi maalum amemuua mwanaharakati mashuhuri wa Kikurdi Mahmud Wali,wanaharakati wamethibitisha.
Taaarifa zingine zimeelezea utata juu ya kutoonekana kwa wawakilishi wawili ambao walirejea uwanja wa ndege wa Syria wakitokea nchini China walikokwenda kujadili kukomeshwa kwa ghasia za Syria.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya