Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-Mapigano-Usalama

Gaza : pendekezo la kusitisha mapigano latupiliwa mbali

Ndege za kijeshi za Israel zimeendelea na mashambulizi ya anga jumanne wiki hii katika ukanda wa Gaza baada ya kusitisha mapigano kwa muda wa saa sita. Pendekezo la kusitisha kwa mapigano lilitolewa na Misri, lakini kundi la Hamas limetupilia mbali pendekezo hilo.

Kifaru cha jeshi la Israel kwenye mpaka wa ukanda wa Gaza, Julai 15 mwaka 2014.
Kifaru cha jeshi la Israel kwenye mpaka wa ukanda wa Gaza, Julai 15 mwaka 2014. REUTERS/Nir Elias
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizo hayo ya anga yamelenga mji wa Khan Younes, kusini mwa Gaza, na mtaa mwengine wa Zaetoun mashariki mwa mji wa Gaza.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) limeelezea masikitiko yake kwa namna nyumba zinavyoharibiwa na kuteketezwa katika ukanda wa Gaza, wiki moja baada ya kulipuka kwa mashambulizi ya Israel ambayo yamesababisha maafa ikilinganishwa na yale ya mwaka 2012.

“Hasara ni kubwa kwa watu na mali”, amesema msemaji wa UNRWA, Sami Mshasha katika mkutano na waandishi wa habari.

Wapelestina wakiwa mbele ya nyumba iliyobomolewa kwa makombora yaliyorushwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.
Wapelestina wakiwa mbele ya nyumba iliyobomolewa kwa makombora yaliyorushwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Mohammed Salem

Mshasha amesema kwamba, kulingana na takwimu ambazo wanazo, watu 174 wameuawa na wengine zaidi ya 1.100 wamejeruhiwa, huku akibaini kwamba idadi hio huenda ikaongezeka.

“Idadi kubwa ya wahanga ni wanawake na watoto”, ameendelea kusema Mshasha.

Hata hivo, amesema , nyumba 560 zimebomolewa pamoja na maelfu ya majengo, huku baadhi yakiwa ni ofisi za Mamlaka ya Palestina.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,  John Kerry.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry. REUTERS/Jim Young

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ameonya kutokea kwa machafuko zaidi katika aridhi ya Israeli na ukanda wa Daza, iwapo Israel na Hamas hawatasitisha mapigano.

Kerry ameamua kutojielekeza nchini Misri, na badala yake atarejea nchini Marekani kuzungumza na rais baracka Obama uwezekano wa kulipa muda na kulifanyia kazi pendekezo la kusitisha mapigano kwa pande husika liliyotolewa na Misri.

“Tuko tayari kufanya kile kiliyo chini ya uwezo wetu ili kusaidia pande mbili kukutana kwa mazungumzo”, amesema Kerry, huku akiwa na imani kuwavmazungumzo yataitikiwa na wote.
Mapigano kati ya Israel na Hamas yamesababisha maafa katika ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.