Pata taarifa kuu
IRAQ-ISIL-MAREKANI-Usalama-Siasa

Iraq : mashambulizi yanaandaliwa dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na ISIL

Raia wa kaskazini mwa Iraq wameanza kuwa na matumaini wakati huu bwawa muhimu la Moussoul, waliyokuwa wakitumia kwa kupata maji na umeme kuondolewa mikononi mwa wapiganaji wa kislamu na kudhibitiwa na wapiganaji wa kikurdi. Washington imepongeza mafanikiyo hayo ya kijeshi.

Wapigani wa kikurdi (Pershemega) wakiwa ktaika uwanja wa vita dhidi ya wapiganaji wa kislamu, Agosti 18 mwaka 2014.
Wapigani wa kikurdi (Pershemega) wakiwa ktaika uwanja wa vita dhidi ya wapiganaji wa kislamu, Agosti 18 mwaka 2014. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

Serikali za Marekani na Iraq pamoja na wakurdi wameapa kuendelea na mapigano dhidi ya wapiganaji wa kislamu, hadi pale watahakikisha wapiganaji wa kislamu wanaondolewa kwenye maeneo wanayoshikilia tangu mwezi Juni mwaka 2014.

Kwa upande wake rais wa Marekani Barack Obama, amesema kwamba operesheni ya kuteka bwawa la Moussoul inaonesha uwezekano wa ushirikiano kati ya wapiganaji wa kikurdi na jeshi la Iraq dhidi ya kundi linalohatarisha usalama wa kanda nzima. Kwa upande wao viongozi wa Iraq wamekua na matumaini makubwa, ya kurejesha kwenye himaya yao Moussoul, mji wa pili wa taifa la Iraq, baada ya kuona kuwa, wapiganaji wa kislamu wametimuliwa katiaka eneo muhimu la bwawa la Moussoul. Mji wa Moussoul ni ngome ya wapiganaji wa kislamu tangu mwezi Juni mwaka 2014.

Hakuna kinacho ashiria kuwa mapigano dhidi ya wapiganaji wa kislamu kwa lengo la kuuteka mji wa Moussoul yataanza hivi karibuni. Tayari wakurdi wamebaini kwamba hawaoni faida ya kuendelea na mapigano dhidi ya wapiganaji wa kislamu kwa lengo la kudhibiti mji mzima wa Moussoul, ambao hauko chini ya mamlaka yao. Wakurdi hao wamepania kuviweka kwenye himaya yao vijiji viliyokua chini ya mamlaka yao, hususan Keyf, kaskazini mwa Iraq, kabla ya kutekwa na wapiganaji wa kislamu.

Hata hivo ushirikiano si mzuri kati ya jeshi la Iraq na wapiganaji wakikurdi, ambapo mara kwa mara wamekua wakihasimiana. Mwishoni mwa juma liliyopita, ujumbe wa wanasiasa wa kikurdi ulijielekeza katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad ili kujadili na viongozi wa Iraq namana ya kuwashirikisha katika serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Bwawa la umeme la Mossoul linaloshikiliwa kwa sasa na wapiganaji wa kikurdi.
Bwawa la umeme la Mossoul linaloshikiliwa kwa sasa na wapiganaji wa kikurdi. AFP PHOTO/AHMAD AL-RUBAYE

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.