Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-MISRI-HAMAS-Usalama

Palestina: Gaza: Hamas yawaua wapalestina 18

Watu kumi na nane, raia wa Palestina, wanaotuhumiwa kushirikiana na jeshi la Israel wameuawa ijumaa wiki hii katika ukanda wa Gaza, ambako kunashuhudiwa mapigano kati ya Israel na hamas, televisheni inayomilikiwa na kundi la Hamas imetangaza.

Kiongozi wa kisiasa wa Hamas Khaled Mechaal.
Kiongozi wa kisiasa wa Hamas Khaled Mechaal. AFP PHOTO/HAMAS-HO
Matangazo ya kibiashara

Sita miongoni mwa watu hao 18, wameuawa hadharani na watu waliokua wamevalia sare za wapiganaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Ezzedine al-Qassam, shirika la habari la Ufaransa limethibitisha.

Mauaji hayo yametekelezwa mbele ya umati wa waumini waliokua wakitokea kudiriki swala ya Ijumaa mbele ya msikiti mkuu wa Gaza.

Kwa mujibu wa mashahidi na mtandao uliyo karibu na Hamas wa Majd, watu wengine kumi na mmoja wameuawa kwa risase karibu na makao makuu ya polisi katikati ya mji wa Gaza. Mwengine mmoja ameuawa karibu ya eneo walikouawa watu hao 11.

Mauaji hayo yanatokea, siku moja baada ya viongozi watatu wakuu wa kijeshi wa Hamas kuuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel dhidi ya jengo moja katika mji wa Rafah (kusini mwa ukanda wa Gaza).

Kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Khaled Meechal (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Khaled Meechal (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas. REUTERS/Mohamed Al Hams/Handout

Wakati hayo yakijiri Amir wa jumuiya waislam nchini Koweit anakutana kwa mazungumzo na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas pamoja na kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Khaled Meechal, wakati huu ambapo mapigano kati ya Israel na Hamas yanaendelea kurindima katika ukanda wa Gaza. Maelfu ya raia wameuawa katika mapigano na wengine wamelazimika kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.