Pata taarifa kuu
HCR-SYRIA-Wakimbizi-Haki za binadamu

HCR yakabiliwa na tatizo la kuhudumia wakimbizi milioni 3 wa Syria

Raia milioni tatu kutoka Syria wanaripotiwa kuyahama makaazi yao, baadhi wamekimbilia nje ya nchi kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Syria na waasi wanaopinga utawala wa Bashar Al Assad.

Watoto kutoka Syria wakipewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi nchini Jordan.
Watoto kutoka Syria wakipewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi nchini Jordan. REUTERS/Muhammad Hamed
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi HCR limebaini kwamba linahitaji Dola bilioni 2 hadi mwishoni mwaka 2014 ili kuwahudumia wakimbizi hao.

Idadi ya wakimbi kutoka Syria imeendelea kuongezeka siku baada ya siku kufuatia mapigano kati ya jeshi la syria na waasi wanaopinga utawala wa Bashar Al Assad. Baadhi ya wakimbizi hao wamelazimika kukimbilia mataifa jirani.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi HCR limesema nusu ya wakimbizi hao kutoka Syria wamefukuzwa katika nyumba zao na kulazimika kukimbilia wakihofia usalama wao.

Mbali ya wakimbizi hao milioni tatu walioorodheshwa na HCR, ambao wamekimbilia nje ya nchi, kuna wakimbizi wa ndani milioni 6.5, wengi wao wakiwa ni watoto. HCR imesema kuna wakimbizi wengine ambao bado wako njiani wakiyakimbia mapigano yanayodumu zaidi ya mwaka mmoja.

Ni kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka 64 likiendesha shughuli zake, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi halijawahi kukabiliana wimbi kubwa la wakimbizi kama hilo. Kwa mujibu wa kamishina mkuu wa shirika la misaada ya kibinadamu, Antonio Guteres, jumuiya ya kimataifa inalazimika kuingilia kati ili kunusuru maisha ya wakimbizi hao kutoka Syria.

Wimbi kubwa hilo la wakimbizi wa Syria limesababishwa na kuongezeka kwa mapigano katika baadhi ya maeneo, hususana katika miji ya Raqaa na Allepo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.