Pata taarifa kuu
SYRIA-ISIL-Mapigano-Usalama

Syria: IS yateka ndege tatu za kivita

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (SOHR), wapiganaji wa Dola la kislam wameteka ndege tatu za kivita, na huenda walipewa mafunzo ya urubani kwenye uwanja wa ndege wa kaskazini mwa Syria.

Mfano wa ndege aina ya MIG-23.
Mfano wa ndege aina ya MIG-23. Creative commons/Piotr Butowski
Matangazo ya kibiashara

Ndege hizo zinasadikiwa kuwa ni aina ya MIG-21 au MIG-23. Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria (SOHR), wapiganaji hao wa Dola la Kiislam huenda wameziteka ndege za kivita za Syria, ziliyokuwa katika eneo la kijeshi wanalodhibiti kwa sasa, katika mikoa ya Raqqa na Aleppo.

SOHR inashuku kwamba huenda marubani walioasi jeshi la Iraq na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam ndio wamekua wakitoa mafunzo ya urubani kwa wapiganaji hao nchini Iraq.

Shirika hilo ambalo limebaini kuwa na vithibitisho, limethibitisha kwamba wapiganaji wa Dola la Kiislam wamekua wakirusha ndege hizo kutoka uwanja mdogo wa ndege za kijeshi wa Al-Jarrah, katika mkoa wa Aleppo, kaskazini mwa Syria.

“ Watu wengi wameziona, zikiruka mara kadhaa zikitokea katika uwanja wa Al-Jarrah”, Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu (SOHR), Rami Abdelrahman ameliambia shirika la habari la AFP.

Taarifa hiyo hajathibitishwa na uongozi wa majeshi ya muungano ambao unaendesha mashambulizi dhidi ya wapiganji wa Dola la Kiislam.

Ndege aina ya MIG-21 na MIG-23 zilitengenezwa nchini Urusi wakati wa vita vya baridi. MIG-23 ilitengenezwa kufanya kazi katika maeneo ya milima na jangwani, na kuendesha mashambulizi ya ardhini. Shirika hilo halijathibitisha iwapo ndege hizo zina uwezo wa kuendesha mashambulizi ya angani kwa kutumia makombora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.