Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINE-Usalama

Israeli: raia wa Jerusalem watiwa hofu ya mashambulizi

Hali ya taharuki imeendelea kutanda katika mji wa Jerusalem. Wayahudi wenye itikadi kali wamepanga kuandamana Alhamisi Novemba 6 wakielekea kwenye Msikiti wa Al-Aqsa, eneo takatifu kwa Waislam.

Mashambulizi kwa kutumia gari ni mbinu mpya ambayo imeanzishwa, kama ilivyotokea Jumatano Novemba 5 mwaka 2014 katika mji wa Jerusalem.
Mashambulizi kwa kutumia gari ni mbinu mpya ambayo imeanzishwa, kama ilivyotokea Jumatano Novemba 5 mwaka 2014 katika mji wa Jerusalem. Reuters/Alex Kolomoisky
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo huenda yakasababisha kuongezeka kwa mashambulizi, kama ilivyokua Jumatano Novemba 5 wakati mji huo ulishuhudia shambulio la gari dhidi ya polisi wa Israeli. Lakini dereva aliuawa wakati alipokua akijaribu kutimka.

Shambulio hilo lilisababisha kifo cha askari polisi wa Israel, na watu wengi kujeruhiwa wakiwemo raia wa kawaida na wanajeshi. Wakati huohuo shambulio jingine la gari lilitokea katika mji wa Cisjordania.

Watu watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo, akiwemo mmoja ambaye ni mautiuti. Shambulio hilo liliyotokea Jumatano jioni wiki hii, lilikua limelenga kundi la wanajeshi waliyokua karibu na makaazi ya walowezi. Baada ya tukio hilo, dereva wa gari alitimka akielekea katika mji wa Palestina wa Hebron. Mtuhumiwa huyo anasakwa wakati huu na polisi ya Israeli, ambayo inamshuku kuwa mfuasi wa Hamas.

Hayo yakijiri hali ya wasiwasi imeripotiwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Novemba 6 katika maeneo ya mji wa Jerusalem yanayokaliwa na Warabu. Makabiliano makali yalitokea kati ya vijana wa Kipalestina na polisi. Inaarifiwa kuwa baadhi ya vijana wa Kipalestina wamekamatwa.

Raia wa Israel waishio katika mji wa Jerusalem wamesema kutiwa hofu na mashambulizi hayo, wakibaini kwamba huenda yakaongezeka, kufuatia maandamano yanayopangwa kufanyika leo Alhamisi novemba 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.