Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-JERUSALEM-Siasa-Usalama

Jerusalem: raia waishi katika "mazingira ya hofu"

Siku moja baada ya shambulio dhidi ya Sinagogi mjini Jerusalem lililogharimu maisha ya watu watano na wangine wengi kujeruhiwa, waisraeli wameanza kua na hofu ya kutokea kwa vita vya mawe (Intifada) katika mji huo.

Mazishi ya watu watatu kati ya watano waliouawa katika shambulio lililoendeshwa Jumanne asubuhi Novemba 18 mwaka 2014 dhidi ya Sinagogi, Jerusalem.
Mazishi ya watu watatu kati ya watano waliouawa katika shambulio lililoendeshwa Jumanne asubuhi Novemba 18 mwaka 2014 dhidi ya Sinagogi, Jerusalem. REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa hatua mpya za kiusalama ziliyochukuliwa, viongozi wa Israeli wametangaza kwamba huenda wakaondoa vikwazo dhidi ya kumiliki silaha viliyokua viliwekewa raia wa Israeli kwa minajili ya kujihami dhidi ya mashambulizi yanayoendeshwa na baadhi ya raia wa palestina.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema atashinda vita dhidi ya mji wa Jerusalem kati yake na Palestina baada ya Wapalestina wawili kuwaua mayahudi wanne wa kiisraeli kwa kuwapiga risasi Magharibi mwa mji wa Jerusalem.

Netanyahu ameahidi kuwa serikali itatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa mauaji hayo yanakoma na inalinda mji wa Jerusalem.

Kwa muda mrefu mji wa Jeruselam umeendelea kuwaniwa kati ya Palestina na Israel, huku kila upande ukisema ni mji wake Mtakatifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.