Pata taarifa kuu
SYRIA-ISRAEL-Mashambulizi-Usalama

Israel yataka kuzuia silaha kutoifikia Hezbollah

Syria imeituhumu Israel kuendesha mashambulizi Jumapili Desemba 7 dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na utawala wa Damascus. Israel inatuhumiwa kuwapa msaada moja kwa moja waasi na wanajihadi.

Yuval Steinitz, Waziri wa ujasusi wa Israel.
Yuval Steinitz, Waziri wa ujasusi wa Israel. REUTERS/Eduardo Munoz/Files
Matangazo ya kibiashara

Israeli haijakiri au kukanusha mashambulizi hayo ya angani, lakini mapema asubuhi, waziri wa ujasusi, Yuval Steinitz, amethibitisha kwamba nchi yake imekua ikijaribu kuzuia silaha kuingia Lebanon zikitokea Syria.

“ Israel imechukua uamzi wa kuzuia silaha ambazo zimekua zikipelekwa kwenye maeneo yanayoshikiliwa na makundi ya kigaidi”, amesema Waziri wa ujasusi, Yuval Steinitz, akihojiwa kwenye redio kuhusu mashambulizi yaliyoendeshwa dhidi ya Syria Jumapili Desema 7. Israel inaichukulia Hezbollah ambayo inaisaidia jeshi la Bashar Al Assad kama kundi la kigaidi. Hezbollah ni adui wake wa kwanza. Kama Yuval Steinitz hatambui kuwa nchi yake iliendesha mashambulizi dhidi ya Syria, ameonesha angalau msimamo wa serikali.

Jeshi la Israeli linadaiwa kuwa limemeendesha mashambulizi kadhaa nchini Syria na Lebanon tangu yaanze machafuko nchini Syria. Mara ya mwisho Israel kuendesha mashambulizi ilikua mwezi februari mwaka 2014. wakati huo Israel iliteketeza msafara wa magari kwenye mpaka wa Lebanon, msafara wa magari ambayo yalikua yakibeba, kwa mujibu wa Israel, makombora yakipelekwa kwenye maeneo yanakaliwa na Hezbollah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.