Pata taarifa kuu

NATO yatamatisha shughuli zake Afghanistan

Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi NATO umeaandaa sherehe za makabidhiano  jijini Kabul nchini Afganiustan, wakati huu majehsi hayo yanapojiandaa kuodoka juma hili.

Jenerali John Campbell, mkuu wa kiosi cha kimataifa cha ISAF, amekaribisha kazi iliyotekelezwa na Nato, wakati wa sherehe za kuondoka kwa kikosi  hicho, Desemba 28 mwaka 2014.
Jenerali John Campbell, mkuu wa kiosi cha kimataifa cha ISAF, amekaribisha kazi iliyotekelezwa na Nato, wakati wa sherehe za kuondoka kwa kikosi hicho, Desemba 28 mwaka 2014. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Makabidhiano hayo yalifanyika kwa usiri mkubwa kutokana na hofu ya kundi la Taliban ambalo limekuwa likitishia kutekeleza mashambulizi jijini Kabul.

Siku ya Jumatano maelfu ya majeshi ya NATO ambayo yamekuwa nchini humo kwa zaidi ya miaka 13 sasa yatarudi nyumbani, na kuliachia jeshi la Afgansitan kuendelea na juhudi za kuelendelea kulinda amani na kupambana na Taliban.

Hata hivyo, wanajeshi wa kigeni 12,500 watasalia nchini humo ili kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Mkuu wa kikosi hicho cha kimataifa ISAF, Jenerali John Campell, amesema kikosi hicho kitaanza kazi tarehe 1 mwezi Januari na pia kitahudumu kama msingo wa majeshi ya NATO na wanajeshi wa Afganistan.

NATO imekuwa na wanajeshi 130,000 kutoka mataifa 50, huku Marekani ikiongoza kuwa na wanajeshi wengi.

Zaidi ya wanajeshi wa NATO elfu nne wamepoteza maisha wakiwa katika vita nchini Afganistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.