Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-UN-Usalama

Abbas aanzisha upya jitihada za kuwepo kwa taifa huru la Palestina

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema anajadiliana na nchi ya Jordan kuwaislisha upya azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka Palestina kutambuliwa kama nchi huru.

Mvutano kati ya Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kushoto) na kiongozi wa Mamlaka ya palestina, Mahmoud Abbas (kulia)..
Mvutano kati ya Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kushoto) na kiongozi wa Mamlaka ya palestina, Mahmoud Abbas (kulia).. Reuters/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Mpango huu wa Palestina unakuja wiki moja tu baada ya Baraza hilo la Umoja wa Mataifa kukataa kupitisha azimio lingine la kuishinikiza Israeli kuacha ujenzi wa maakazi katika maeneo ambayo Palestina inasema ni yake.

Akizungumza mjini Ramallah mwishoni mwa juma lililopita rais Abbas amesema kuwa ana imani kuwa dunia itaihurumia na kusisitiza kuwa hatachoka kuendelea kutafuta uhuru wa Palestina.

Wiki iliyopita, rais Abbas aliomba Palestina kujiunga na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, uamuzi ambao uliukasirisha Israel.

Serikali ya Israel, kwa upande wake, imesisitiza kuwa haitaruhusu kamwe wanajeshi wala maofisa wake kufikishwa mbele ya Mahakama kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kwa tuhuma za kuhusika na makosa ya uhalifu wa kivita kwenye eneo la ukanda wa Gaza.

Tangazo la waziri mkuu Netanyahu linakuja saa chache baada ya serikali yake kutangaza kuzuia kiasi cha dola milioni 127 zinazotokana na utozwaji wa ushuru kwa ajili ya Serikali ya Palestina.

Mohammed Shtayyeh ni msuluhishi wa zamani wa mamlaka ya Palestina, amebaini kuwa serikali ya Israel inastahili kuwajibika kwa makosa ya kivita na sio serikali yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.