Pata taarifa kuu
URUSI-IRAN-MAUZO-USALAMA

Putin aondoa vikwazo vya silaha kwa Iran

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru Jumatatu wiki hii kuondolewa kwa vikwazo vya silaha Urusi iliyoiwekea Iran kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Vladimir Putine ametoa idhni ya kuiuzia Iran mifumo ya ulinzi dhidi ya makombora S-300.

Mifumo ya ulinzi dhidi ya makombora S 300 , katika mitaa ya Moscow, wakati wa mafunzo kwa ajili ya gwaride ya kijeshi, Mei mwaka 2009.
Mifumo ya ulinzi dhidi ya makombora S 300 , katika mitaa ya Moscow, wakati wa mafunzo kwa ajili ya gwaride ya kijeshi, Mei mwaka 2009. REUTERS/Alexander Natruskin
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Marekani imepokea uamzi huo wa Urusikwa shingo upande, ikibaini kwamba mauzo hayo “ hayatasaidia lolote”. Israeli pia imelani uamzi huo wa Urusi.

Uamzi wa kuichukulia Iran vikwazo vya kutoiuzia makombora S-300 ulichukuliwa mwezi Septemba mwaka 2010 na rais wa zamani wa Urusi Dmitri Medvedev. Mkataba wa dola milioni 800 ulitiliwa saini mwaka 2007. Hata hivyo uamzi wa mtangulizi wa rais Vladimir Putin ulichukuliwa katika kutekeleza azimio 1929 la Umoja wa Mataifa unaoiadhibu Iran kwa mpango wake tata wa nyuklia.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergueï Lavrov amebaini kwamba wakati huo Kremlin ilienda mbali na majukumu yake, na kwa sasa imelazimika kuondoa vikwazo hivyo.

" Tunaamini kwamba katika hatua ya sasa, hakuna haja ya aina hii ya vikwazo, hasa ikiwa ni uamuzi ambao Urusi iliuchukua kwa hiari yake, na hakuna hoja nyingine. Itakumbukwa kwamba S-300 ni kombora tu ya kujihami, ambayo haitumiwi kwa mashambulizi, na haihatarisha hali yoyote katika Ukanda, ikiwa ni pamoja na Israeli", amesema Sergueï Lavrov.

Lavrov ameongeza kuwa : " Kutokana na hali ya wasiwasi inayojiri katika Ukanda huo, kama ilivyoshuhudiwa na maendeleo ya haraka ya matukio ya wiki iliyopita nchini Yemen, mifumo ya kisasa ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya anga ni muhimu sana."

Vikwazo hivyo vya silaha dhidi ya Iran, vilizua uhasama katika uhusiano kati ya Moscow na Tehran. Wakati huo Iran iliwasilisha mashtaka yake mbele ya Mahakama ya kimataifa ikiomba Urusi kulipa fidia ya dola bilioni 4.

Kwa sasa Moscow ina imani kwamba mgogoro huo umekwisha na iko mbioni kufufua mahusiano mazuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wakati huohuo Israel imelani uamzi huo wa Urusi wa kuiondolea Iran vikwazo vya kuiuzia makombora S-300. “ Iran inaruhusiwa kujidhatiti kijeshi na kununua silaha za maangamizi kuliko kuilazimisha iachane na shuguli zake za kigaidi katika Mashariki ya Kati”, amesema waziri wa Israeli mwenye dhamana ya ujasusi, Yuval Steinitz.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.