Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HUTHI-VITA-SIASA

Waasi wa huthi wataka kusitishwa kwa mashambulizi ya anga

Karibu saa 24 baada ya kutangazwa kwa uamzi wa kusitishwa kwa mashambulizi ya anga nchini Yemen, hali bado ni tete. Waasi wa Huthi wanadai mashambulizi ya anga yasitishwe mara moja kabla ya kuanza mazungumzo yoyote.

Ndege ya jeshi la Saudi Arabia ikishiriki katika mashambulizi dhidi ya waasi wa Huthi, Yemen, Aprili 2 mwaka 2015.
Ndege ya jeshi la Saudi Arabia ikishiriki katika mashambulizi dhidi ya waasi wa Huthi, Yemen, Aprili 2 mwaka 2015. REUTERS/Saudi Press Agency
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo wa kusitishwa kwa mashmbulizi ya anga hautachukua muda mrefu. Ingawa Operesheni inayojulikana kama " Dhoruba yenye maamuzi " ya muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kumalizika rasmi, ndege za kivita za Saudi Arabia zilirejea Jumatano wiki hii kwenye kituo cha jeshi la anga la Yemen. Ndege hizo zilishambulia ngome za wanamgambo wa Kishia waliovamia na kudhibiti kambi ya jeshi, karibu na mji wa Taiz kusini-Magharibi mwa Yemen.

Pamoja na tangazo la kusitisha kwa mashambulizi ya anga lililotpolewa Jumanne usiku, Riyadh ilizingatia kuweka mambo sawa: nia ya Saudi Arabia ni kuyapa nafasi mazungumzo na masuala ya siasa, wamesema viongozi wa Saudi Arabia. Shughuli za kijeshi hata hivyo bado zipo. Waasi Huthi wanafuatiliwa kwa karibu na iwapo wataendesha shambulio lolote ndege za kivita za muungano wa Kirabu hazitosita kuingilia kati.

Hata hivyo waasi wa Huthi wamepinga utaratibu huo unaopendekezwa na Saudi Arabia, wakibaini kwamba huenda hawawezi kushiriki mazungumzo ya kisiasa wakati bado wanahofu ya kushambuliwa au kukamatwa. Waasi hao wameomba kusitishwa kwa mashambulizi ya anga mara moja kabla ya kuanza kwa mazungumzo yatakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Mashahidi wamesema mapigano bado yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Yemen.

Wakati huohuo Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini Yemen, huku mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha siku tisa zilizopita.

Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni upelekaji wa huduma za kitabibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.