Pata taarifa kuu
ISRAELI-SIASA

Israel: Benjamin Netanyahu ashinikizwa

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ana masaa machache tu ya kuunda serikali yake. Tarehe ya mwisho ni Jumatano wiki hii usiku wa manane.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Nishati, katika kikao cha Bunge, tarehe 4 Mei mwaka 2015.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Nishati, katika kikao cha Bunge, tarehe 4 Mei mwaka 2015. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu huyo, ambaye alishinda uchaguzi wa wabunge wa Machi 17, amekua akizungumza na vyama kadhaa vya kisiasa tangu mwezi mmoja na nusu uliyopita kwa minajili ya kujiunga na muungano wake. Lakini majadiliano yamekua magumu zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Baada ya uchaguzi, Benjamin Netanyahu aliahidi kuunda muungano katika kipindi cha wiki tatu. Mwezi mmoja na nusu baadaye umekamilika, mungano huo ukiwa bado haujaundwa. Waziri Mkuu, ambaye hawezi kutawala na chama chake pekee cha Likud, kutokana na kushindwa kupata wabunge wengi katika Baraza la Bunge, amekua akitafuta washirika. Lakini washirika hawo hawajapatikana kutokana na kila mmoja amekua akitia mbele maslahi yake binafsi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Jerusalem, Murielle Paradon, kila mshirika ambaye Benjamin Netanyahu alikua akipata, alikua akitaka apewe nyadhifa muhimu katika serikali. Na hiyo ndio sababu mpaka sasa washirika hawo hawajapatikana.

Mmoja wa washirika wa kudumu wa Netanyahu, Avigdor Lieberman, mwenye msimamo mkali, ameamua kushiriki katika serikali itakayoundwa katika misingi ya "utendaji kazi na usawa", amesema kiongozi wa chama cha kizalendo cha Israeli Beiteinu.

Kwa sasa, waziri mkuu ameunganisha vyama viwili vya Ultra-Orthodox vyenye msimamo mkali pamoja na chama cha mrengo wa kati. Endapo akivishirikisha vyama vya kidini kutoka jamii ya Wayahudi katika muungano wake, atakuwa na idadi kubwa ya wabunge. Lakini wingi huo utakua hauna umuhimu wowote, kutoakana na sauti moja tu, ambayo itafanya serikali yake kudhoofika zaidi.

Kama Netanyahu atashindwa Jumatano jioni kupata idadi ya vyama vinavyohitajika ili aweze kuunda serikali yenye nguvu, rais wa Israel anaweza kumpa mtu mwengine majukumu ya kuunda serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.