Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-MAPIGANO-USALAMA

Ramadi mikononi mwa IS

Baada ya mji wa Ramadi, nchini Iraq kudhibitiwa na kundi la wanamgambo wa Dola la Kiislamu IS, wanamgambo hao wameimarisha ulinzi katika mji huo mkuu wa jimbo la Al Anbar, ulio kwenye umbali wa kilomita 100 magharibi mwa Baghdad.

Vikosi vya usalama vya Iraq, katika mji wa Ramadi, Aprili 9 2015.
Vikosi vya usalama vya Iraq, katika mji wa Ramadi, Aprili 9 2015. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Watu mia tano wanasadikiwa kuwa wameuawa ndani ya kipindi cha siku mbili za mapigano, na wengine zaidi ya 8000 wameukimbia mji huo.

Mpaka sasa, kundi la wanamgambo wa Dola la Kiislamu wanadhibiti vituo vyote vya kijeshi na polisi katika mji wa Ramadi, kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi nchini Iraq. Kwa mujibu wa afisaa huyo, jeshi , polisi na kikosi cha polisi kinachopambana dhidi ya ugaidi pamoja na washirika wao wameondoka katika mji wa Ramadi.

Msemaji na mshauri wa mkuu wa jimbo la Al Anbar, amethibitisha kuwa mji huo umeanguka mikononi mwa wanamgambo wa kiislamu wa IS.

Umoja wa Mataifa umelaani hatua hiyo wanamgambo wa IS wa kuudhibiti mji wa Ramadi. Wakati huo huo waziri mkuu wa Iraq Haider Al Abadi amesema kuwa wanajipanga kwa sasa kwa kushirikiana na majeshi ya Kishia ili kukabiliana na wapiganaji hao wa IS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.