Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-mazungumzo-SIASA

Mazungmzo ya amani ya Yemen yatazamiwa kuanza Geneva

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuzindua mazungumzo ya kisiasa nchini Yemen, utafanyika juma lijalo jijini Geneva nchini Uswizi.

Shawarma mpaka kati ya Saudi Arabia na Yemen, ambapo mapigano yameendelea kushuhudiwa.
Shawarma mpaka kati ya Saudi Arabia na Yemen, ambapo mapigano yameendelea kushuhudiwa. Clarence Rodriguez/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya amani ya Yemen lakini hadi sasa haijafahamika ni kina nani watakaoshiriki katika mkutano huo.

Tangazo hili limekuja wakati huu operesheni inayoongozwa na Saudi Arabia ikiendelea dhidi ya waasi wa Kihuthi.

 Abdullah al-Mualami Balozi wa Saudi Arabia katika Umoja wa Mataifa amesema ana uhakika Iran haitaalikwa katika mazungumzo hay yatakayofanyika tarehe 28 mwezi huu.

Wanajeshi wa Saudi Arabia wakishrikiana na washirika wake walinza tena mashambulizi ya angaa dhidi ya waasi wa Kihuthi nchini Yemen tangu mwishoni mwa jumalililopita.

Mashambulizi haya mapya yanakuja baada ya kumalizika kwa muda wa siku tano wa kusitisha mapigano ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa wa mapigano hayo.

Wanasiasa nchini Yemen wamekua wakijadiliana kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa suluhu ya kisiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.