Israel: "hakuna kuwavumilia Wayahudi wenye msimamo mkali"
Israel imesema haitowavumilia Wayahudi wenye msimamo mkali ambao wamekua wakijihusisha na vitendo viovu dhidi ya raia wa palestina.
Imechapishwa:
Uamzi huo unakuja baada ya kijana mmoja kuchomwa kisu na Myahudi mmoja mwenye msimamo mkali wakati wa sherehe ya mashoga jijini Jerusalem Alhamisi juma lililopita, Kijana huyo amefariki Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita.
Baada ya machafuko yaliyotokea siku za hivi karibuni, serikali ya Israel imechukua hatua dhidi ya Wayahudi wenye msimamo mkali.
Baraza la usalama la kitaifa nchini Israel limekutana Jumapili Agosti 2 ili kutathmini athari za shambulio lililotokea katika kijiji cha Douma, kaskazini mwa Cisjordania, na lile llililoptokea wakati wa sherehe ya mashoga jijini Jerusalem. Mawaziri wametoa idhni kwa vikosi vya usalama ili wachukuwe hatua zinazohitajika kwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa mashambulizi hayo.
Shambulio la kigaidi
Aina hii ya kukamatwa itatekelezwa baada ya kupitishwa na mshauri wa serikali anayehusika na maswala ya sheria ambaye atajadiliana na Mwendesha mashtaka mkuu wa jamhuri. Israel imelaani pia shambulio lililosababisha kifo cha mtoto mchanga Ali Dawabcheh. Israel imetaja shambulio hilo kuwa ni la kigaidi.