Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-KIFUNGO-SHERIA

Israel: Mahakama Kuu yafuta kifungo cha Mohammed Allan, raia wa Palestina

Mfungwa kutoka Palestina Mohammed Allan uamzi wake wa kususia chakula aliouchukua tangu miezi miwili iliyopita akipinga kufungwa bila kuhukumiwa.Ameyasema hayo mwanasheria wake.

Maandamano ya kuunga mkono Mohammed Allan, Agosti 19, 2015 katika mji wa Hébron.
Maandamano ya kuunga mkono Mohammed Allan, Agosti 19, 2015 katika mji wa Hébron. REUTERS/Mussa Qawasma
Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii Mahakama Kuu ya Israel imefuta kifungo alichokuemo Mohammed Allan, kutokana na hali yake ya afya.

Uamzi wa kufutwa kwa kifungo hicho umechukuliwa na Mahakama Kuu, lakini kwa sasa Allan Mohammed bado amelazwa hospitalini. Hali yake ya afya ni mbaya sana. Uchunguzi wa afya uliowasulishwa Mahakama Jumatano wiki hii umeonyesha raia huyo wa Palestina amepata matatizo kwenye ubongo kutokana na uamzi huo wa kususia chakula aliochukua kwa kipindi cha miezi miwili.

Wakati wa kesi hiyo ikisikilizwa, wanasheria wa Mohammed Allan waliomba mteja wao aachiliwe huru mara moja, wakati ambapo wawakilishi wa serikali ya Israel walisema kuwa kuharibika kwa ubongo hakutorekebishwa ili mtu huyu asiwi tishio na achiliwe huru. Allan Mohammed anatuhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic Jihad, kundi linalochukuliwa na Israel kama la kigaidi.

Raia huyo wa Palestina mwenye umri wa miaka 30, ambaye ni mwenye taaluma ya uanasheria alichukua uamzi wa kususia chakula ili kupinga kufungwa kwake bila kufunguliwa mashitaka. Mamia ya raia wa Palestina wamekua wakizuiliwa jela nchini Israel bila hata hivyo kufunguliwa mashitaka. Kesi hii ya Allan imekuwa ikihamasisha wananchi wa Palestina na imekuwa ni tatizo kubwa kwa mamlaka ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.