Pata taarifa kuu
YEMENI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Yemen: zaidi ya watu 20 wauawa katika Msikiti wa Washia Sanaa

Watu wasiopungua ishirini wameuawa na 50 kujeruhiwa Jumatano wiki hii katika mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga dhidi ya Msikiti wa Washia katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, vyanzo vya kimatibabu vimebaini katika ripoti mpya.

Mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaendeshwa katika Msikiti wa Washia katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, kwa mujibu wa mashahidi.
Mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaendeshwa katika Msikiti wa Washia katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, kwa mujibu wa mashahidi. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo hivi hapo awali vimearifu kuwa watu wanane wameuawa na thelathini kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ambayo yalilenga Msikiti wa Washia wa eneo la Jarraf, baada tu ya Sala ya jioni.

Yemen imeendelea kukumbwa na machafuko kati ya makundi hasimu hususan waasi wa Kishia na wanajeshi wanaomuunga mkono rais wa nchi hiyo aliyekimbilia nchini Saudi arabia Mansour Hadi wakishirikiana na wanamgambo pamoja na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.

Machafuko hayo yanayoendelea kushuhudiwa nchini Yemen yamesababisha vifo vya watu wengi na malfu wengine kujeruhiwa na wengine kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.