Pata taarifa kuu
YEMEN-MASHAMBULIZI-USALAMA

Muungano wa Kiarabu wapata pigo kubwa katika vita nchini Yemen

Falme za Kiarabu na Bahrain wamepoteza Ijumaa wiki hii askari 50 ikiwa ni pamoja na askari 45 kutoka Falme za Kiarabu na watano kutoka Bahrain.

Mawingu ya moshi mweusi juu ya jengo la Wizara ya Ulinzi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, wakati wa mashambulizi ya anga ya muunagano wa kiarabu, Septemba 4, 2015.
Mawingu ya moshi mweusi juu ya jengo la Wizara ya Ulinzi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, wakati wa mashambulizi ya anga ya muunagano wa kiarabu, Septemba 4, 2015. AFP PHOTO / MOHAMMED HUWAIS
Matangazo ya kibiashara

Kuuawa kwa askari hawa ni pigo kubwa tangu nchi hizi zilipokubali kuanzisha vita katika muungano wa kiarabu chini ya uongozi wa Saudi Arabia ambayo imeendelea kupata upinzani katika vita dhidi ya waasi wa Kishia wa Huthi.

Tangu mwanzo, mwishoni mwa mwezi Machi, mashambulizi ya anga ya muungano, kwa kumuunga mkono rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi dhidi ya waasi, Falme za Kiarabu zimepoteza jumla ya askari wake 52.

Jeshi la UAE lilitangaza awali vifo vya askari 22 waliouawa kwa mujibu wa vyanzo vya Yemen na mlipuko katika ghala ya zana katika jimbo la Marib, mashariki mwa mji wa Sanaa.

Akari ishirini na tatu waliojeruhiwa walifariki muda mfupi baadaye, na kupelekea kufikia idadi ya askari 45 kutoka Emirati ambao wamesha uawa, shirika la habari la serikali WAM limearifu.

Licha ya pigo msiba huo, Mwanamfalme mrithi wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, ambaye pia ni mkuu wa vikosi vya kijeshi, amesema katika tweet "uamuzi" wa nchi yake kuendelea kutoa " msaada wake kwa ndugu wa Yemen dhidi dhuluma na uchokozi."

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa imetangazwa nchini Emirati. wakati huo huo Ijumaa jioni ndege za jeshi la nchi hiyo ziliendesha mfululizo wa mashambulizi dhidi ya ngome za waasi na maeneo ya kijeshi katika katika miji ya Marib, Sanaa, Saada (kaskazini), ngome kuu ya waasi wa Huthi na Ibb (katikati), kwa mujibu wa shirika la habari la serikali (WAM).

Ofisi ya Rais nchini Yemen imetangaza kuwa askari watano wa Bahraini wameuawa pia katika mlipuko huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.