Pata taarifa kuu
UN-PALESTINA-USHIRIKIANO

Palestina mbioni kupandisha bendera yake kwenye makao makuu ya UN

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umepitisha kwa kiasi kikubwa rasimu ya azimio linaloiruhusu Palestina kupandisha bendera yake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na Ufaransa wamepiga kura ya ndio kwa azimio la kuiruhusu Palestina kupandisha bendera yake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na Ufaransa wamepiga kura ya ndio kwa azimio la kuiruhusu Palestina kupandisha bendera yake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. REUTERS/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

Rasimi hiyo imepitishwa kwa kura 119 dhidi ya kura 8, huku wajumbe 45 wa mMkutano Mkuu huo wakijizuia kutoa msimamo wao.

Hatua ya ziada katika kampeni kubwa ya kidiplomasia ambayo Mamlaka ya Palestina imekua ikiendesha ili kuona kwamba taifa lake laweza kutambuliwa kimataifa.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu mjini New York, Marie Bourreau, hii ni hatua ya kiishara kwani Palestina inaendelea kubaki kama taifa lisilokuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifalicha ya kushiriki mikuntano ya Umoja huo. Lakini ishara hiyo inaelezea mambo mengi kuhusu nia ya Wapalestina ili kuharakisha utambuzi wa taifa lao wakati ambapo mchakato wa amani umeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu.

Nchi nyingi wanachama, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, hata hivyo zimeeleza kuwa kura zao zinakwenda sambamba na azimio hili katika nia njema ya kutoa shinikizo kwa ufumbuzi kwa nchi mbili, ambazo ni Palestina na Israel. " Kutokuchukua hatua si chaguo ", amesisitiza Balozi wa Ufaransa, François Delattre.
Israel, kwa upande wake, imewatuhumiwa Wapalestina kwa kuwateka nyara maafisa wa Umoja wa Mataifa kwa hatua hiyo ya " kiishara lakini isiyokua na nguvu yoyote."

Marekani, ambayo imepiga kura ya hapana dhidi ya nakala hiyo, imesisitiza kwamba kupandisha bendera haipaswi kuwa mbadala kwa mazungumzo, ambayo kwa sasa yamesitishwa.

Umoja wa Mataifa kwa sasa ina siku 20 kwa pandisha bendera ya Palestina, yenye rangi nyekundu, nyeusi, nyeupe na kijani, kabala ya kuwasili kwa Rais Mahmoud Abbas katika Mkutano Mkuu ujao wa tarehe 30 Septemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.