Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MSF-TALIBAN-USALAMA

MSF yasitisha shughuli zake katika mji wa Kunduz

Shirika la kimataifa la Madaktari wasio na mipaka MSF, limesema kuwa limejiondoa kutoka mji wa Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan baada ya hospitali yake kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani.

Vikosi maalum vya Afghanistan katika mji wa Kunduz, Sepemba 29, 2015.
Vikosi maalum vya Afghanistan katika mji wa Kunduz, Sepemba 29, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

MSF imesema hatua ya wanajeshi wa Marekani na Afganistan kushambulia hospitali hiyo kwa tuhma kuwa wapiganaji wa Taliban walikuwa ndani, imewashangaza sana.

Afisa wa mawasiliano wa shirika hilo, Kate Stegeman, amesema miongoni mwa watu ishirini na wawili waliouawa, kumi na mbili ni wafanyakazi wa shirika hilo, MSF.

Stegeman, amesema wagonjwa wote walioonekana mahututi wamehamishiwa kwenye vituo vingine vya afya na kwamba hakuna mfanyakazi wa shirika lao hilo aliebakia katika mji wa Kunduz.

Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi hili.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon pia ametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi hili.

Mwishoni mwa juma lililopita, serikali ya Afganistan ilisema kuwa Hospitali hiyo ya MSF ilikuwa inatumiwa kuwapa hifadhi wapiganaji wa Taliban.

Shambulizi hilo limesababisha MSF kuwaondoa wafanyikazi wake katika kituo hicho.

Kwa sasa wanajehsi wa Afganistan wanadhibiti mji wa Kunduz baada ya kuwoanda Taliban kwa msaada wa wanajeshi wa NATO.

Kumeshuhudiwa hali mbaya ya wasiwasi tangu mji wa Kunduz kuangukia mikononi mwa wapiganaji wa kundi la Taliban mapema wiki iliyopita, ambapo maduka yameharibiwa katika mapigano yanayoendelea.

Hata hivyo wiki iliyopita serikali ya Afghanistan ilitangaza kwamba mji huo umerejeshwa kwenye himaya yake kutoka mikononi mwa waasi wa Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.