Pata taarifa kuu
YEMEN-MASHAMBULIZI-USALAMA

Yemen: watu 13 wauawa katika mashambulizi Sanban

Kwa uchache watu 13 waliokua wakihudhuria katika sherehe ya harusi wameuawa na wengine 38 kujeruhiwa katika shambulio lililoendeshwa katika mji wa waasi wa Sanban, unaopatikana zaidi ya kilomita mia moja kusini mwa Sanaa, chanzo cha hospitali kimeeleza Alhamisi wiki hii.

Wakazi karibu na eneo lililoshambuliwa na muungano wa Kiarabu, tarehe 1 Oktoba, 2015 katika mji wa Sanaa, Yemen.
Wakazi karibu na eneo lililoshambuliwa na muungano wa Kiarabu, tarehe 1 Oktoba, 2015 katika mji wa Sanaa, Yemen. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi shambulizi hilo, ambalo limelenga nyumba ambamo kulikua kukifanyika sherehe ya harusi, limeendeshwa na ndege za muungano wa kiarabu unaosaidia serikali ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia ambayo inajaribu kijeshi tangu mwishoni mwa mwezi Machi kuzuia waasi wa Huthi, wanaoungwa mkono na Iran, kuchukua udhibiti kamili baada ya kuingia kwao katika mji wa Sanaa, mwaka mmoja uliopita.

" Hospitali ya Dhamar Hospitali imepokea miili 13 na majeruhi 38 baada ya shambulizi la mabomu dhidi ya nyumba ambapo watu kadhaa walikuwa wakisherehekea harusi ", kilisema chanzo cha hospitali.

" Ndege za muungano zimeendesha shambulizi. Nyumba yote imeteketea ", Taha al-Zuba, mkaazi wa Sanban amesema.

Wiki iliyopita, muungano wa kiarabu unaopambana dhidi ya waasi ulikanusha kushambulia kwa mabomu ukumbi wa harusi katika mji wa Mokha, uliyoko kusini magharibi mwa Yemen, kwenye bahari ya Shamu, ambao unadhibitiwa na waasi wa Kishia wa Huthi. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 131.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.