Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-MASHAMBULIZI

Israel-Palestina: jaribio la mashambulizi kwa kutumia bisibisi

Alhamisi hii, raia mmoja wa Palestina amejaribu kuwashambulia kwa bisibisi askari wa Israel katika eneo la kukagua magari karibu na mji wa Hebron, kusini mwa Ukingo wa Magharib, kabla ya kuuawa, jeshi la Israel limearifu.

Vikosi vya usalama vya Israel karibu na mwili wa Mpalestina aliyeuawa kwa kujaribu kuendesha shambulio dhidi ya askari wa Israel mjini Hebron, Desemba 24, 2015.
Vikosi vya usalama vya Israel karibu na mwili wa Mpalestina aliyeuawa kwa kujaribu kuendesha shambulio dhidi ya askari wa Israel mjini Hebron, Desemba 24, 2015. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mpalestina aliye kuwa amejihami kwa bisibisi alisogelea eneo la kukagua magari karibu na mji wa Hebron, na kujaribu kushambulia vikosi vya usalama. Askari walijibu shambulio hilo kwa haraka, na kumpiga risasi mshambuliaji, ambaye alifariki papo hapo", jeshi limesema katika taarifa yake.

Hilii ni shambulio la pili linaloendeshwa na Wapalestina ndani ya masaa kadhaa katika Ukingo wa Magharibi, nchini Israel. Shambulio la kwanza, lililoendeshwa karibu na mji wa Hebron, lilipelekea mshambuliaji, ambaye ni raia wa Palestiina kuuawa. Hata hivyo mshambuliaji huyo kabla ya kuuawa alikua amewajeruhi vikali walinzi wawili karibu na eneo la Ariel.

Tangu Oktoba 1, wimbi la ghasia linaloikumba Israeli na maeneo mbalimbali ya Palestina limesababisha vifo vya watu 127 upande wa Wapalestina, 19 upande wa Waisrael, ikiwa ni pamoja na Mmarekani mmoja na raia mmoja wa Eritrea, kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la aUfaransa la AFP.

Idadi kubwa ya Wapalestina waliouawa ilitokana na kutekeleza ao kujaribu kutekeleza mashambulizi kwa kutumia visu lakini pia kwa kutumia gari na bunduki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.