Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Mkutano kati ya Abbas na Netanyahu wawezekana?

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jumatatu hii kuwa yuko tayari kukutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ili kuzungumzia amani na kuwa ameweka kando ratiba yake ya wiki hii kwa ajili ya mkutano huo.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mwenzake rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mwenzake rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas Reuters
Matangazo ya kibiashara

Netanyahu amesema amefanya hivyo kufuatia hotuba ya Rais wa mamlaka ya Palestina Mafmoud Abbasaliyoitoa Alhamisi wiki iliyopita kwenye runinga ya Israel.

"Hivi karibuni, nilimsikia Rais Abbas kwenye runinga ya Israel akisema kwamba kama mimi nikimualika, atakuja," Netanyahu amesema katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Lubomir Zaoralek.

"Kama nilivyosema asubuhi ya leo kwa ujumbe kutoka Congress ya Marekani, ninamualika kwa mara nyingine tena. Nimeweka kando ratiba yangu kwa wiki hii. Anaweza kuja siku yoyote, nipo hapa ntampokea," Netanyahu amesema.

Mahmoud Abbas na Benjamin Netanyahu hawajakutana hadharani tangu mwaka 2010, kwa mujibu wa vyombo vya habari. Mikutano isiokuwa ya hadhara iliarifiwa na vyombo vya habari. Wawili hawa walikutana mwezi Novemba 2015 katika mkutano kuhusu Tabia nchi katika mji wa Le Bourget (Ufaransa) na walifurahishwa kuona wanapeana mkono.

Jitihada za kutatua mgogoro wa zamani wa miongo kadhaa zimeshindikana tangu kushindwa kwa juhudi za Marekani mwezi Aprili 2014. Ardhi ya Palestina, Jerusalem na Israel zinapitia wimbi la ghasia ambazo zimesababisha vifo vya Wapalestina 200 na Waisrael 28 tangu Oktoba 1, kulingana na takwimu zinazotolewa na shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Pande hizi mbili zinatupiana lawama juu ya ukosefu wa mazungumzo. Bw Netanyahu anasema mara kwa mara kuwa yupo tayari kwa minajili ya kuanzishwa kwa mazungumzo bila masharti.

Abbas kwa upande wake anasema kuwa yuko tayari kujadili, ikiwa ni pamoja na kanuni ambazo si masharti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.