Pata taarifa kuu
SYRIA-OBAMA-MAPIGANO

Obama apinga kupelekwa kwa askari wa nchi kavu Syria

Serikali ya Syria na waasi wako tayari kupambana, baada ya kusitisha mapigano kwa kipindi cha wiki nane.

Rais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano na waandishi wa habari  katika Ikulu ya White House, Aprili 5,2016.
Rais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Aprili 5,2016. REUTERS/Gary Cameron
Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii, Aprili 24, watu 26 wameuawa katika mashambulizi, katika jimbo la Aleppo (kaskazini mwa nchi), lakini rais wa Marekani amepinga uwezekano wowote wa kutumwa kwa askari wa nchi kavu kwa lengo la kupatia ufumbuzi vita vinavyoendelea nchini humo.

Kwa uchache watu 26 wameuawa Jumapili hii katika mashambulizi yalioendeshwa na jeshi la serikali na waasi katika mji wa kaskazini wa Aleppo, unaokumbwa na machafuko kwa siku tatu mfululizo.

Tangu Ijumaa, watu 63 wameuawa katika mji mkuu wa zamani wa kiuchumi wa Syria, ambao unakabiliwa kwa sasa na mashambulizi ya angani na makombora yanayorushwa baada ya kipindi cha wiki nane cha utulivu kutokana na mkataba wa usitishwaji mapigano ulianzishwa na Marekani na Urusi na kuanza ktekelezwa tarehe 27 Februari.

Jumapili makomborayalirushwa na wapiganaji dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na serikali na kuua watu 10, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja na watoto wawili, Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limebaini.

serikali ya Rais Bashar al-Assad imeijibu kwa mlolongo wa mashambulizi ya angani katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi, mashambulizi ambayo yameghaimu maisha ya watu 16, kwa mujibu wa OSDH.

Kumi na mbili miongoni mwa watu hawo walipoteza maisha katika mashambulizi dhidi ya soko la mboga katika kitongoji cha Sakhour na wanne katika vitongoji vingine vya waasi, OSDH imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.