Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Mapigano yakoma Aleppo

Hali ya utulivu imeshuhudiwa Alhamisi hii katika jimbo na mji wa Aleppo nchini Syria baada ya Marekani na Urusi kufikia mwafaka wa kusitisha mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Uharibifu mkubwa uliosababishwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi Aleppo.
Uharibifu mkubwa uliosababishwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi Aleppo. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Syria limesema litatii mkataba huo ambao unatarajiwa kushuhudiwa kwa siku mbili zijazo.

Rais Bashar Al Assad hata hivyo amesema hatakubali wanajeshi wake kushindwa katika mji huo uliopo Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waangalizi wa maswala ya Haki za Binadamu wanasema wakazi wa mji huo wameonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida na hakujashuhudiwa mashambulizi yoyote ya anga.

Urusi na Marekani wanataka kurejesha haraka iwezekanavyo mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika mji huo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilithibitisha usiku wa Jumatano hii makubaliano kati ya Washington na Moscow juu ya ujenzi wa mji wa Aleppo na usitishwaji wa mapigano.

Moscow itaongeza mara mbili jitihada zake za kumshawishi rais wa Syria Bashar al-Assad kwa kuzingatia mkataba huu. Washington, kwa upande wake, itafanya hivyo kwa upinzani. Mgawanyo huu wa majukumu kati ya nchi hizi mbili tayari ulipelekea kuhitimisha mkataba wa ndani katika mkoa wa Latakia na Damascus, ni mpango huu unapaswa kufuatwaili kupunguza ukali wa mapigano na mashambulizi katika jimbo la Aleppo.

Imekua ni siku kadhaa, karibu wiki, ambapo Urusi na Marekani walikuwa wakiwasiliana moja kwa moja kufikia usitishwaji wa uhasama na hasa zaidi, kupanua mikataba ya kurejesha utulivu iliyoafikiwa siku kumi zilizopia, kwa mkoa wa Damascus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.