Pata taarifa kuu
UFARANSA-ISRAEL-PALESTINA

Ayrault afutilia mbali shutuma za Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault amekamilisha ziara yake katika Mashariki ya Kati ambako alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Benjamin Netanyahu (kushoto) na Jean-Marc Ayrault wakipeana mkono Jumapili hii Mei 15, 2016 katika mkutano katika ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Jérusalem.
Benjamin Netanyahu (kushoto) na Jean-Marc Ayrault wakipeana mkono Jumapili hii Mei 15, 2016 katika mkutano katika ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Jérusalem. REUTERS/ MENAHEM KAHANA
Matangazo ya kibiashara

Bw Ayrault amejaribu kutetea jitihada ya nchi yake na kuanzisha upya mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina, siku chache tu kabla ya mkutano mjini Paris.

Kutetea kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati ilikuwa changamoto kwa Jean-Marc Ayrault. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amekua akitambua msimamo wa Israel kwa kupinga jambo hilo. Lakini mbali na hilo, alikabiliwa na shutuma za Waziri Mkuu wa Israel Binjamin Netanyahu.

Waziri Mkuu wa Israel amelaani "upendeleo" wa Ufaransa, baada ya utata juu kupigia kura azimio moja kwa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Utamaduni na Sayansi (UNESCO), azimio ambalo kwa mujibu wa Israel halitambui uhusiano wa kihistoria kati ya Wayahudi na Msikiti wa Al-Aqsa, sehemu takatifu kwa Waislamu.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo ya upendeleo, Jean-Marc Ayrault amesema hakutaka "kuingia katika kuzungumzia kuhusu neno hili au lile." "Ufaransa haiwajibiki, amesema, lakini akiamini kwamba kama haitawezekana kufanikisha fikra za kundi la Kiislamu la Daech (IS) katika Ukanda huo, kunahitajika kufanyika jambo fulani."

Jean-Marc Ayrault ametetea jitihada ya Ufaransa ya kuitisha mkutano wa kimataifa kufufua mchakato wa amani, pengine katika majira ya Joto. mkutano wa maandalizi umepangwa kufanyika Mei 30 katika mji wa Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.