Pata taarifa kuu
Michezo

Alieshambuliwa na mashabiki wa Chelsea kupewa mualiko

Mwaka mmoja baada ya kukumbwa na mkasa wa ubaguzi wa rangi dhidi ya mashabiki wa clubu y Chelsea ya nchini Uingereza katika barabaraza za reli jijini Paris, Souleymane Sylla, amealikwa kuhudhuria mechi ya marudio ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Chelsea na Paris Saint Germain itayopigwa Jumanne ijayo.

Suleymane Sylla raia wa Paris aliendeshewa kitendo cha ubaguzi wa rangi
Suleymane Sylla raia wa Paris aliendeshewa kitendo cha ubaguzi wa rangi
Matangazo ya kibiashara

Sylla mwenye Asili ya visiwa vya Ile Maurice mwenye umri wa miaka 33 baba wa watoto 3 ambae alishambuliwa wakati akipanda kwenye treni na kundi la mashabiki wa clabu ya Chelsea waliodaikuwa wao ni wabaguzi na ndicho kinacho wafurahisha.

Sylla atahudhuria mchezo wa ligi ya ya mabingwa baada ya kupokea mualiko kutoka kwa Kundi linalo pambana na ubaguzi.

Sylla ameliambia gazeti la kila siku la Le Parisien kwamba amepokea mualiko kutoka kwa shirika la SOS racism, hivyo lazima ashiriki ilikuwaonyesha waliomshambulia kwamba bado yupo licha ya kwamba jeraha alilolipata kutokana na shambulio hilo bado halijapona.

Wahusika wa tukio hilo walikana kuhusika na mashambulizi hayo, lakini mkanda wa video umewaumbua na kudhirisha wazi namna walivyomshambulia Sylla.

Richard Barklie, mwenye umri wa miaka 50 afisa wa polisi zamani, Joshua Parsons, mwenye umri wa miaka 20 na William Simpson, mwenye umri wa miaka 26 walipewa adhabu ya kutohudhuria mechi za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano huku Jordanie Munday, mwenye umri wa miaka 20, akipewa adhabu ya kutoshuhudia mechi kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.