Pata taarifa kuu
Michezo

Kocha wa Zamalek Ahmed Mido afutwa kazi

Mchezaji mshambuliaji wa zamani wa klabu za Tottenham na Middlesbrough za nchini Uingereza, Ahmed ‘Mido’ Hossam amefutwa kazi ya ukocha katika klabu ya Zamalek ya Misri siku 37 tu baada ya kukabidhiwa mikoba rasmi ya kukionoa kikosi hicho kwa mara ya pili.

Mido, kocha wa Zamalek aliefutwa kazi
Mido, kocha wa Zamalek aliefutwa kazi Reuters/Amr Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Mido mwenye umri wa miaka 32 ambaye awali mwaka 2014 alipewa kibarua cha kufundisha soka katika kilabu hiyo bingwa ya Misri kwa mkataba wa miezi 6 alirejeshwa tena kufundisha timu hiyo mwezi Januari mwaka huu kabla ya kufutwa tena.

Kocha Mido alishinda michezo yake minne ya kwanza akiwa na Zamaleck lakini dosari ilianzia pale timu hiyo ilipotoka sare katika mchezo mmoja na kufuataiwa na kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Al Ahly hiyo jana.

Sare na kipigo hicho imesababisha kocha huyo kupigwa kalamu huku timu yake ikiwa imeachwa pointi 7 na timu ya Al Ahly inayoongoza ligi kuu ya soka nchini Misri.

Mkurugenzi Mpira wa Klabu hiyo Hazem Emam ambaye aliteuliwa pamoja na Kocha Mido naye amefutwa kazi huku Mohamed Salah akitangazwa kuwa kocha wa mpito kuchukua nafasi ya Mido wakati klabu hiyo ikiangalia uwezekano wa kuajiri kocha kutoka nje.

Mido aliyechukua nafasi ya kocha kutoka Brazil Marcos Paqueta,kabla ya kupigwa kalamu amekua kocha wa tatu kufukuzwa kazi na Zamaleck kwa msimu huu akiwemo Jesualdo Ferreira na Paqueta.

Mido alistaafu kucheza soka mwaka 2013 na akaanza kazi yake ya kwanza ya ukocha kwenye klabu za zamaleck januari 2014 na baadaye akondolewa kutokana na matokeo yasiridhisha na hatimaye akarudishwa januari mwaka huu kabla ya kufutwa tena hii akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa siku 37.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.