Pata taarifa kuu
EURO 2012

Chama cha wachezaji ulimwenguni chaonyesha wasiwasi wa kuwepo vitendo vya kibaguzi wakati wa michuano ya EURO 2012

Umoja wa shirikisho la wachezaji wa mpira wa miguu duniani FIFPro, umesema kuwa unahofu kuwa baadhi ya wachezaji wake toka barani ulaya huenda wakafanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi wakati wa fainali za EURO 2012.

Uwanja wa Dariusz Boczek ulioko nchini Poland ambao utatumika kwaajili ya michuano ya EURO 2012
Uwanja wa Dariusz Boczek ulioko nchini Poland ambao utatumika kwaajili ya michuano ya EURO 2012 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa shirikisho hilo Theo van Seggelen, amesema kuwa kwa uchunguzi na uzoefu ambao wamekuwa wakishuhudia kwenye michuano mingi ya kombe la mataifa ya Ulaya, wachezaji wengi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Kiongozi huyo ametolea mfano mechi ambazo zitapigwa nchini Ukrain akisema kuwa nchi hiyo imekithiri kwa mashabiki wake kuwa na otovu wa nidhamu hasa kwa kuendekeza vitendo vya kibaguzi.

Seggelen ameongeza kuwa kwa mtazamo wake anadhani nchi ya Ukrain haikupaswa kupewa nafasi ya kuandaa fainali hizo kutokana na historia ya mashabiki wake wengi wa soka kuwa na ubaguzi kwa baadhi ya wachezaji.

Ripoti ya shirikisho hilo imeonesha kuwa asilimia 9 ya wachezaji wanaocheza soka barani ulaya wameripoti kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa soka toka nchini Ukrain.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.