Manchester United  - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 05 juni 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 05 juni 2012

Manchester United yamsajili Shinji Kagawa kutoka Borussia Dortmound

Shinji Kagawa mchezaji mpya wa Manchster United

Na Victor Melkizedeck Abuso

Klabu ya soka ya Uingereza, Manchester United imekubali kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa.

Kagawa mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akichezea soka yake kulipwa katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmound.

Mchezaji huyo tayari amepata kibali cha kufanya kazi na madaktari wa klabu hiyo wamethibitisha kuwa hali yake ya afya ni nzuri.

Kagawa amesajiliwa  kwa Pauni Milioni 12 kutokana na kile klabu ya Manchester United inasema mchezaji huyo ameonesha kiwango cha juu cha soka nchini Ujerumani.

Kati ya mechi 31 ambazo Kagawa amecheza katika ligi ya Ujerumani,amefunga mabao 13 katika msimu wa ligi kuu mwaka uliopita.

Manchester United pia ilitarajiwa  kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard ambaye aliamua kwenda kuichezea klabu ya Chelsea.

Machster United walimaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya soka msimu uliopita.
 

tags: Chelsea - Ligi Kuu Nchini Ujerumani - BUNDASLIGA - Manchester United
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close