Ufaransa-Uingereza -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatatu 11 juni 2012 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 12 juni 2012
Ufaransa kuchuana na Uingereza michuano ya Euro 2012
Wachezaji wa ufaransa wakiwa mazoezini jana Juni 10
REUTERS/Nigel Roddis
Timu ya taifa ya Ufaransa inashuka uwanjani jumatatu hii kupepetana na Uingereza katika michauo ya kombe la Ulaya inayoendelea nchini Ukraine Polande. Vijana wa Laurent Blanc wamesema wapo tayari kupambana kuhakikisha wanaibuka washindi katika mechi yao hiyo ya kwanza katika michuano hiyo.
Wakati Ufaransa wanakutana na Uingereza, wenyeji wa michuano hiyo Ukraine wataipokea Sweden katika mechi ya pili. Hapo jana Italia ilikwenda sare ya kufungana bao moja kwa moja na Uhispania







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya