Pata taarifa kuu
EURO 2012

Timu ya taifa ya Ureno na Ujerumani zatinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Euro 2012

Michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya maarufu kama EURO 2012 imeendelea kutimua vumbi kule nchini Ukrain na Poland na kushuhudia vigogo mbalimbali wakisonga mbele huku wengine wakiaga mashindano hayo.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani wakishangilia mara baada ya ushindi wa jana
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani wakishangilia mara baada ya ushindi wa jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mechi za hapo jana ilishuhudiwa viwanja viwili nyasi zake zikiwa kwenye patashika kwa nchi ya Ujerumani kuwa wenyeji wa Denmark wakati Ureno walikuwa wakikipiga na timu ya taifa ya Uholanzi.

Mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu za Ureno na Uholanzi ambapo kwenye mechi hiyo ikashuhudiwa timu ya taifa ya Ureno ikisonga mbele kwenye michuano hiyokwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1.

Uholanzi ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao lililofungwa kiufundi na mchezaji Rafael van der Vaart kabla ya Christian Ronaldo kuandika bao la kusawazisha kabla ya timu hizo kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu lakini walikuwa ni Ureno ambao walitumia nafasi zao vizuri na kupata bao la pili lililofngwa tena na Christian Ronaldo.

Katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Ujerumani ilikuwa ikipepetana na timu ya taifa ya Denmark baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja na hivyo kukata tiketi ya kucheza robo fainali.

Kwa matokeo ya hapo jana yanamaanisha timu za Ureno na Ujerumani zimetinga hatua ya robo fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.