Uingereza - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 03 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 03 agosti 2012

Fabrice Mwamba kuanza tena mazoezi

Fabrice Muamba.
Fabrice Muamba.
Clive Brunskill/Getty Images

Na Ali Bilali

Fabrice Muamba, amerejea tena kucheza soka baada ya kuanguka na kupoteza fahamu katika mchezo wa ligi kuu nchini Ungereza na timu ya Bolton Marchi 17 mwaka huu.

Fabrice Mwamba amezungumza na kituo cha habari cha televisheni ya Marekani CNN kwamba alipokuwa likizo huko Dubai katika hoteli moja, na baadae kusikia watu wanacheza soka, na baadae nilijiunga nao na kucheza dakika kati ya 20 na 25.

Mchezaji huyo wa Uingereza mwenye asili ya DRCongo, amesema alijisikia faraja sana ambapo kwake ilikuw akama mazoezi. Fabrice mwamba mwenye umri wa miaka 21 amesema anataji kwamba Mwenyezi Mungu atamsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida na kurejea tena uwanjani kama kawaida.

 

tags: Ligi Kuu Nchini Uingereza - Uingereza
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close