TANZANIA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumapili 19 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumapili 19 agosti 2012

Simba B yaibuka kidume,yaibamiza Mtibwa sugar 4-3

Kikosi cha Simba B cha Tanzania kimetwaa ubingwa dhidi ya Mtibwa
Kikosi cha Simba B cha Tanzania kimetwaa ubingwa dhidi ya Mtibwa
thehabari.com

Na Martha Saranga Amini


Kikosi cha pili cha timu ya Simba kimeonesha umwaba baada ya kuutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC SUP8R kwa kuilaza Mtibwa sugar kwa mabao 4 kwa 3 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Dakika 120 za mchezo zilimalizika kwa matokeo hayo baada ya kushuhudia Edward Christopher kuanza kuifungulia Simba bao la awali katika dakika ya 12 baada ya kumshangaza kipa wa Mtibwa langoni mwake,huku goli lingine likizamishwa kimiani dakika ya 32 ambapo Mtibwa sugar ilisawazisha bao la awali.

Kwa ushindi huo,Simba imejinyakulia kitita cha milioni 40 pamoja na medali,sambamba na mchezaji wale Edward Christopher akizawadiwa milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora huku Mtibwa ikiondoka na milioni 20 pamoja na medali.
 

tags: Tanzania
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close