Pata taarifa kuu
Brazili

Brazil yajivuta katika Orodha ya Viwango vya FIFA

Brazil imeendelea kuwa nje ya Orodha ya nchi kumi kwa viwango vya ubora vya FIFA vya hii leo huku uingereza, Denmark na Ugiriki zikionekana kuwa vinara.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Brazili
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Brazili
Matangazo ya kibiashara

Brazil iliyokuwa nafasi ya 13 Mwezi uliopita, imepanda juu nafasi moja hatua iliyoifikia baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Sweden wakati wa Mechi ya Kirafiki nchini Sweden.
Nafasi hiyo imeshangaza ikilinganishwa na ushindi wa Mechi 10 kati ya 13 za kimataifa zilizopigwa Mwaka jana.
 

Uingereza imeendelea kushika nafasi ya tatu, nafasi ambayo waangalizi wa mambo wanaeleza kuwa ni nafasi ya juu kupewa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
 

Uhispania iki kileleni, juu ya Ujerumani ambao walijiangusha baada ya kupoteza mchezo wake na Argentina kwa kupigwa Magoli 3-1 katika Mechi ya kirafiki Mwezi uliopita.
 

Orodha ya Msimamo wa Viwango vya FIFA

1. Uhispania Spain
2. Ujerumani
3. Uingereza
4. Ureno
5. Uruguay
6. Italia
7. Argentina
8.Uholanzi
9. Croatia
10. Denmark
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.