michezo - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 08 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatatu 10 septemba 2012

Sharapova nje, Azarenka kumvaa Serena Williams

Maria Sharapova atolewa na Victoria Azarenka
Maria Sharapova atolewa na Victoria Azarenka
Reuters/Nir Elias

Na Martha Saranga Amini

Bingwa nambari moja duniani katika mchezo wa tennis kwa upande wa kina dada Victoria Azarenka, ambaye alipata kuwika katika michuano ya Australian Open, ataingia katika mpambano kujaribu bahati yake katika hatua ya fainali za michuano ya Us Open baada ya kumtoa Maria Sharapova.

Katika mechi ya marudio ya fainali za Australian Open ambapo alifanikiwa kumchapa Sharapova na kushinda taji ya mashindano hayo, kwa magoli ya seti 3-6, 6-2, 6-4.

Azarenka amesema alifanya jitihada ili kunyakua fursa ya kwanza lakini pia Maria amemsifu Maria kuwa ni mchezaji mzuri ambaye alifanya jitihada ambazo zilimpa changamoto wakati fulani.

Katika hatua ya fainali jumamosi Azarenka atamkabili Mmarekani Serena Williams, ambaye naye amejiwekea rekodi nzuri katika ulingo wa tennis kwa upande wa kinadada ulimwenguni.
 

tags: Serena Williams - US Open
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close